MWALIMU ANASWA AKIWAFANYIA WANAFUNZI MTIHANI WA DARASA LA SABA HUKO IRINGA
Jeshi
la polisi mkoani Iringa linamshikilia mwalimu wa shule ya msingi
Makungu wilaya ya Mufindi Bw Edwin Ambukile kwa tuhuma za kuwasaidia
majibu wanafunzi wa darasa la saba katika mtihani wa Taifa wa
kuhitimu elimu ya msingi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Bw Ramadhan Mungi (pichani) amesema kuwa tukio hilo limetokea Septemba 15 mwaka huu.
Alisema
kuwa mwalimu huyo ambae ni mwalimu wa masomo ya Sayansi katika shule
hiyo pia alikuwa ni mwalimu wa masomo ya ziada ( katika shule hiyo na
sababu ya kuwasaidia wanafunzi majibu ni kutaka kupata umaarufu kwa
wanafunzi watano aliokuwa akiwafundisha masomo ya ziada aliopata
kuwaahidi kuwa watafaulu mtihani huo.
Alisema
kuwa mwalimu huyo tarehe 11 septemba alipokea mitihani kutoka kwa
msimamizi na baada ya hapo akafungua bahasha ya masomo ya Sayansi na
kuanza kufanya mwenyewe na majibu kuyatuma kwa Sms kwa mke wake .
Hata
hivyo siku ya mtihani mmoja kati ya wanafunzi waliopata majibu hayo
alipoingia katika chumba cha mtihani alionekana akitetemeka kupita
kiasi na hivyo msimamizi wa mitihani alipompekua alimkuta na majibu
hayo na kueleza jinsi alivyosaidiwa na mwalimu huyo .
Kamanda
wa polisi alisema siku ya mtihani mwalimu Ambukile alipangiwa
kusimamia shule ya msingi Igomaa na sasa amekamatwa na atafikishwa
mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.
No comments:
Post a Comment